May 15, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kesho kitakuwa na kibarua kizito kitakapokabiliana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa Kmbe la Shirikisho Afika.

Wapinzani wa Yanga tayari wamewasili jana nchini kwa ajili ya mchezo huo wa pili katika hatua ya makundi ya mashindano haya.

Kuelekea mechi hiyo, Yanga itakosa huduma ya mchezaji wake, Said Makapu kutokana na kutumikia adhabu ya kadi 2 za njano ambazo kwa mujibu wa kanunu za mashindano, mchezaji anapaswa kukosa mechi moja endapo atafikisha idadi ya kadi hizo.

Yanga itamkosa Makapu katika mtanange huo huku ikitakiwa kupambana kupata matokeo ambayo yataitengeneza mazingira mazuri ya kuendelea kusalia kwenye michuan hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kuelekea mechi hiyo, salehjembe.blogspot.com inawatakia kila la kheri Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

4 COMMENTS:

  1. Naungana na Saleh Jembe kuwatakia YANGA kila la heri

    ReplyDelete
  2. Tufuteni machozi watanzania Yanga

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. If Prison 2 Yanga 0 and Mtibwa 1 Yanga 0 that means 2+1 = 3 Therefore, Rayon 3 Yanga 0.
    I will all the Best Rayon Sports

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic