May 7, 2018



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kuwa hajakimbia nje ya nje kujificha bali ameenda kwa ajili ya matibabu.

Poppe amesema kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikieleza kuwa ametoroka na kutimkia nje ya nchi baada ya kupata tetesi kutokana na sakata linalowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva pamoja na Makamu wake, Nyange Kaburu ampapo ametajwa kuunganishwa kwenye kesi hiyo.

Mkuu huyo wa kitengo cha Usajili Simba, ameeleza yupo India hivi sasa akipata matibabu ya goti la mguu wake baada ya kufanyiwa operesheni Novemba mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kufanya naye mahojiano mafupi likitaka kujua kuhusu amri iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, iliyotolewa Aprili 30 2018 ikimtaka akamatwe na afikishwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

Poppe ameeleza kuwa bado hajapata taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo, bali amekuwa akiona tu mitandaoni ikiandikwa kuwa anahitajika kuripoti.

Ikumbukwe awali kab­la ya kuongezwa Poppe na mwenzake, Aveva na Kaburu walikuwa wa­nakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 (Sh 683,115,000) za Kimarekani kabla ya kuongezewa mengine matano na kufikia kumi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic