May 7, 2018



Uongozi wa Klabu ya Yanga umeweka bayana kuwa utamalizana na wachezaji wake juu ya malimbikizo ya fedha zao muda mfupi baada ya kurejea kutoka nchini Algeria ambako kikosi hicho kilienda kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga jana Jumapili ilikuwa nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wake huo wa Kombe la Shirikisho Afrika kupambana na wenyeji wao USM Alger ambapo kikosi hicho kiliwa­kosa nyota wake saba wa kikosi cha kwanza kutokana na matatizo mbalimbali huku ikitajwa wengine waligomea safari hiyo kutokana na kudai fedha zao.

Wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo ni pamoja na Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi, Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.

Akizungumzia juu ya hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alisema kuwa wanatambua nyota wao wanaidai fedha klabu yao lakini wanapam­bana kuhakikisha wanamalizana nao muda mfupi baada ya kikosi hi­cho kurejea kutokea nchini Algeria.

“Tunajua kwamba wachezaji wetu wanadai fedha zao lakini kama uon­gozi tunapanga namna ya kumali­zana nao kwa ajili ya kuwapa stahiki zao, na tumepanga muda mfupi baada ya kurejea nchini tukitoka Algeria basi tuwalipe kile ambacho wanatakiwa kupewa.

“Kama uongozi tunapambana kwa kila namna kuona tunawapa fedha zao japo ilitakiwa wachezaji wapam­bane kuona timu inafika hatua za mbali katika kombe hili kwa ajili ya kuingiza fedha nyingi zaidi ambazo zitarahisisha wao kupata malipo mazuri zaidi,” alisema mwenyekiti huyo.

CHANZO: CHAMPIONI

5 COMMENTS:

  1. pumbafu mnakera sana kwanini hamuwalipi pesa wachezaji hadi wanafikia hatua ya kjugomea match

    ReplyDelete
  2. Mbona mnatuchanganya mara marelia mara mimba,mara baada ya wiki mbili.kumbe mpunga viongozi kuweni wakweli msije kuchomewa vibanda na wananchi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Eti mara mimba, kumbe ndo mana wanatema mate uwanjaniπŸ€”

      Delete
  3. Aibu hiyo walipeni wachezaji haki zao sio sahihi kuwataka wacheze tuuu bila kuwalipa

    ReplyDelete
  4. Hivi hii Klabu haina Mhasibu???
    Inashindwa kuweka bajeti yakueleweka??? Inasajili wachezaji bila kuwa na mipango ya ulipaji mishahara??? Inaniboa sana. Kwanini viongozi wa Kiafrika wengi wanakuwa wazembe hivi???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic