May 7, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia Mkurungenzi wake, Festo Sanga, umetamba kuvunja rekodi ya Simba kutopoteza mechi hata moja msimu huu.

Kikosi cha Singida kitakuwa kinaikaribisha Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania utakaopigwa Jumamosi ya Mei 12 2018 kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Sanga ameeleza kuwa Simba wasitegemee mteremko kwenye mechi hiyo kutokana na namna wanavyozidi kujipanga hivi sasa kuelekea mtanange huo.

Mkurugenzi huyo anaamini Singida italipiza kisasi walichokipata katika mchezo wa raundi ya jijini Dar es Salaam.

Singida itakuwa inaikaribisha Simba ikiwa ina kumbukumbu ya kulala kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam uliopigwa January 18.

Vinara Simba watakuwa wanahitaji alama moja pekee kwenye mchezo huo ili kutangaza kubeba ubingwa baada ya kuukosa kwa takribani miaka mitano.

6 COMMENTS:

  1. Hata mechi yadar walisema wamekuja kuchukua point 3kwa simba.tusubiri mda utaongea.

    ReplyDelete
  2. Kwa mini Singida United mnakuwa na maneno sana, au mnafikiri no Njombe Mji hao?

    ReplyDelete
  3. Hebu ficheni ujinga wenu singida

    ReplyDelete
  4. Simba wekeni nia na dhamira ya kweli hapana kucheza kwa mzaha wafungeni magoli 3 hivi hawa Singida

    ReplyDelete
  5. jamani jamani huu sio mwaka wa utani kabisa watusamehe simba haichi mtu mzima ni mwendo mdundo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic