TAMKO LA UONGOZI WA YANGA BAADA YA NGOMA KUJIUNGA NA AZAM FC
Na George Mganga
Baada ya uongozi wa Azam FC kutangaza rasmi kuwa wameingia mkataba wa awali wa mwaka mmoja na Mzimbambwe, Donald Ngoma, uongozi wa Yanga umesema umesikitishwa zaidi na kitendo alichokifanya mchezaji huyo.
Ngoma aliyekuwa akiitumikia Yanga tangu mwaka 2015 hakuweza kucheza takribani mechi za msimu mzima unaomalizika hivi sasa (2017/18) kutokana na kuwa majeruhi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa Ngoma hajafanya jambo la kiungwana na limemuumiza yeye kama kiongozi kwa kuamua kuondoka kimyakimya bila mawasiliano na uongozi wake.
"Naweza kusema Ngoma hajafanya kitendo cha kiungwana hata kidogo, nimeumizwa kwa kitendo chake cha kuondoka na kuhamia klabu nyingine, yote kwa yote namtakia kheri huko alipohamia" amesema Nyika.
Hiki karibuni uongozi wa Yanga kupitia Nyika ulisema utafanya maamuzi magumu kuhusiana na Ngoma kutokana na kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha.
Ngoma alisajiliwa na Yanga akitokea FC Platnumz ya nchini kwao Zimbambwe na kuweza moja ya wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo, na hii ni kutokana na umahiri wake aliokuwa akiuonesha ndani ya Uwanja.
Kaumia akiwa mchezaji wenu na mkamtenga kutokana nae kwuwa hakufaeni ana majaraha bila ya kumtafutia matibabu. Azam wamempokea na anapelekwa nje kwa matibabu halafu mnasema alichofannya Ngoma si ubinaadamu jee ubinaadamu ni huko kutomjali na kumtenga. Kweli ulimi hauna mfupa. Mtu amwacha mke bila ya sababu halafu anakuja mtu mwenye heri nae n kumuoa halafu unasema mwanamke huyo hana heri je mlitaka Ngoma awew ndio mwisho kimpira na kimaisha? Mmechelewa na kwenu hakuna dhamana
ReplyDeleteAMA KWELI NDIO ULE MSEMO WA WAZEE WAKALIE ULIOSEMA, SAMAKI AKIOZA USIMTUPE UMTAFUTIE VIUNGO UMKAUSHE. ATAKUJA KUNUOKOTA MWENZIO ULIE UJE UJUTE
ReplyDeleteHivi mlitaka Ngoma afanyeje zaidi?
ReplyDeleteDuh makubwa...leo YANGA imekuwa hayo tena.Kweli tunahitaji viongozi wenye digrii.
ReplyDeleteKWI..KWI...KWI..SIZITAKI MBICHI HIZO.TUTASAJILI KINA ADAM SALAMBA NA WACONGOMAN
ReplyDeleteMisishangai maana hata niyonzima alikua akicheza na maumivu kaenda simba kapatiwa matibabu
ReplyDelete