May 25, 2018


Kiungo mahiri wa Yanga, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe, amefunguka kuwa ugumu wa ratiba na kucheza muda mfupi baada ya mechi moja ndiyo sababu pekee ya timu hiyo muda mwingine kugawa pointi kwa wapinzani wao.

Kiungo huyo wa zamani wa FC Platinum ya Zimbabwe, msimu huu kwake haukuwa mzuri kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini

hivi karibuni alirejea dimbani na kuisaidia timu yake kupata ushindi mbele ya Mbao FC ya Mwanza, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Jumanne ya wiki hii.

Kwa sasa Yanga inakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 51, huku ikiwa imebakiza michezo miwili mkononi wa leo Ijumaa itacheza dhidi ya Ruvu Shooting na Azam FC ambao watamaliza nao ligi Jumatatu ijayo.

Akizungumzia juu ya hilo, Kamusoko ambaye ni hodari wa kupiga mipira ya adhabu ndogo (free kick), amesema kwamba kitendo cha wao kucheza michezo mfululizo bila ya kuwa na muda wa kupumzika kimeweza kuchangia kutopata matokeo mazuri lakini akiweka bayana kwamba wao siyo wa kwanza kupitia kipindi kigumu cha kupata matokeo mabaya.

“Yanga ina mashabiki wengi ambao wao kwao kila mechi wanataka ushindi, lakini suala hili la kushindwa kupata matokeo linazitokea timu nyingi sana ukiwaangalia hata Real Madrid walipata matatizo kama haya ya kushindwa kupata matokeo.

“Lakini pia suala la kucheza ndani ya muda mfupi napo kunachangia, sisi tulicheza na Mwadui mkoani Shinyanga kisha tukasafiri na kupumzika kidogo kisha tukacheza na Mbao FC jijini Dar, miili nayo inahitaji mapumziko ya muda mrefu, lakini kwetu tutaendelea kupambana kwenye mechi zilizobaki,” alisema Kamusoko.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic