May 25, 2018

AKIWA NA PRISCILLA

Nyota wa zamani wa FC Barcelona, Ronaldinho yuko katika hatua za mwisho kufunga ndoa na wanawake wawili kwa wakati mmoja.

Ronaldino ,38, ameamua kuwaoa wapenzi wake hao wawili ambao ni Priscilla Coelho na Beatriz Souza na wote ameishawavisha pete ya uchumba.

BEATRIZ

Taarifa kutoka Brazil zimeeleza kwamba, Ronaldinho amekuwa akiishi na wapenzi wake hao wawili katika jumba lake la kifahari jijini Rio de Janeiro.

Ronaldinho amekuwa akiishi na wapenzi wake hao wawili katika jumba hilo lenye thamani ya pauni million 5.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil amekuwa akiwapa pauni 1,500 kila mwezi kwa ajili ya matumizi yao binafsi na warembo hao wameeleza kuelewana.

Gazeti la O Dia la Brazil, limeeleza kwamba wamekubaliana na ndoa itafungwa wakiwa wote watatu.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic