Kapombe aliyeifungia bao Simba katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza, amekuwa mchezaji bora baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa timu hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Simba.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam leo baada ya kuitwanga Singida bao 1-0 jana, ili kujiandaa na mechi dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba wameweka rekodi ya kuchukua ubingwa bila kupoteza msimu huu na sasa wanataka kumalizia ligi bila kufungwa pia.
Kapombe yupo sawa kwa sasa. Labda niweke sawa maelezo yangu yakwamba Kapombe yupo vizuri tangu anachipukia ila hapo kati alifikwa na mitihani ya kidunia. Masuala ya kwenda ufaransa na kurudi aidha kwa hiari yake mwenyewe au ghilba za walimwengu kulimchanganya kwa kiasi fulani. Halafu kukaja kutokea masuala ya majeraha kwa kweli alifikwa na mitihani ila Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wenye nizamu na adabu ya mpira na ni mwenye kukumumbuka fadhila . Wanamsimbazi tuna kila sababu ya kujivunia aina ya mchezaji kama kapombe. Upambanaji wake kwa timu licha ya kutoka kwenye majeraha mazito ni kielelezo tosha yakuwa Simba haikufanya kosa kumrejesha kapombe kundini. Simba imelea vijana wengi na sasa wametapakaa timu mbali mbali nchini na wengi wao wanafanya vizuri kwenye zile timu na asilimia kubwa ya hawa vijana licha yakuwa wanatafuta ajira lakini ni vijana wenye mapenzi na Simba vile vile sasa ingekuwa busara kabisa kwa Simba linapokuja suala la usajili la wachezaji hawa vijana ambao waliwahi kukuzwa na Simba wakapewa kipao mbele ya kuwasajili. Hao akina Mabaraka Yusufu ni figisu tu lakni ile ni haki miliki ya Simba. Sasa hawa akina Kyombo,Miraji Adam,akina Salamba na Bonaventure na wengineo ni kuwarejesha Nyumbani Msimbazi ikiwezekana. Kwani kwa sasa nia na nguvu tunayo ya kufanya hivyo.
ReplyDeleteRejeeni nyumbani kumesheheni na kunona. Msiwache mbachao kwa msala upitao na nguo ya kuazima haisitiri ....... walisema waliotutangulia
ReplyDelete