YANGA WAKO TAYARI KUIMALIZA MTIBWA LEO
Baada ya kushindwa kuutetea ubingwa wake, kikosi cha Yanga kinateremka dimbani Jamhuri Stadium jioni ya leo kucheza na Mtibwa Sugar.
Tayari Yanga wako tayari kwa mchezo huo kufuatia kufanya mazoezi ya mwisho jana katika Uwanja wa Jamhuri Stadium utakaotumika leo huko Morogoro.
Meneja wa kikosi hicho, Hafidh Saleh, amesema kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri kukipiga na Mtibwa leo.
Yanga inaingia kusaka alama tatu za heshima kufuatia kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 2-0 Uwanja wa Sokoine.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo itarushwa mbashara na Azam TV.
0 COMMENTS:
Post a Comment