May 29, 2018


Na George Mganga

Katibu wa mipango wa zamani wa klabu ya Yanga, Abdul Sauko, amewaomba wanachama wa klabu hiyo kujitahidi walau kwenda na kiasi cha shilingi 30,000 katika mkutano mkuu utakaofanyika Juni 10 2018.

Sauko ambaye aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga ametoa ushauri huo kwa wanachama kwenda na kiasi hicho cha fedha ili zikaweze kutumika kwa ajili ya kufanyia usajili wa wachezaji.

Akizungumza kupitia Radio EFM katika kipindi cha Sports HQ, Sauko ameeleza kuwa klabu yao inapitia wakati mgumu kiuchumi hivi sasa huku akisema hakuna mwingine atakayeweza kuikoa zaidi ya wanachama wenyewe.

Mbali na kusaidia suala la usajili, Sauko pia amependekeza wanachama wabebe fedha hiyo itakayoweza kutumika kwa mambo mengine ya klabu kutokana na tatizo la kuyumba kiuchumi linaloikabili Yanga kwa sasa.

Yanga inaenda kufanya mkutano huo ambao awali ulipangwa kufanyika tarehe 16 Juni 2018, siku ambayo inaweza ikawa ni sikukuu ya Idd hivyo ikabidi urudishwe nyumba mpaka tarehe 10 Juni.

4 COMMENTS:

  1. Daaaah!!!! Kweli Yanga maji ya shingo, hata kwenye vikao kunakuwa na kiingilio cha 30,000/= ili kufanya usajili au posho za wachezaji wanaowadai?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  2. Mchezaji gani atakubali kusajiliwa kwa pesa za kuomba misaada na za mishahara zitatoka wapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesahau au unajisahaulisha kwamba mishahara hulipwa na Spoti Pesa?

      Delete
  3. Sauko namuheshimu sana lakini hili analolileta yeye kwani bado ni kiongozi wa Yanga? Analileta kama nani? Mbona Katibu Mkuu yupo na hajasema hilo? Mbona tunadhalilishana bila sababu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic