May 29, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameweka wazi sababu ya watani zake wa jadi Yanga kushindwa kufanya vizuri msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

Rage ameeleza kuwa Yanga imekumbwa na tatizo kubwa la kuwa na wachezaji majeruhi ambao wameweza kuigharimu timu kushindwa kufanya vizuri.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba, amesema Yanga walipaswa kuwafanyia vipimo vya afya wachezaji wao ili kuweza kujua kama wapo fiti kuweza kutumika katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa.

Aidha, Rage ameeleza kuwa pesa si sababu iliyosababisha Yanga kufikia hatua waliyonayo hivi sasa kwasababu wanapata kutoka kwa mdhamini ambaye pia anatoa mpunga wake kwa Simba ambaye ni SportPesa.

Kutokana na hali hiyo, Rage amezishauri timu zingine kufanya vipimo vya afya kwa wachezaji wanaowasajili ili kuepuka matatizo kama ambayo Yanga wameyapata kwenye msimu huu.

Yanga imepokwa ubingwa na Simba msimu huu kwa kufikisha pointi 52 ikiwa nafasi ya tatu huku Azam FC ikishika ya pili kwa kujikusanyia alama 58.

Wakati huo Simba ambao ni mabingwa wapya wamemaliza msimu wakiwa na pointi 69 na wakiweka rekodi ya kuchukua ubingwa wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, japo wakishindwa kumaliza ligi bila kufungwa kufuatia kipigo dhidi ya Kagera.

4 COMMENTS:

  1. hawajapoteza ila wamefungwa hahaha unachokiandika unajua mwenyeww

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duuh! Ni nini kisichoeleweka hapo? Halafu unakuta mtu huyu ni mshabiki wa Barça aka sapota wa Liverpool kwenye mechi yao dhidi ya Real Madrid. Pole sana. Ils sijui ni nini kiliwazuia kuchekelea na kufurahia Majimaji kutoka sare na Simba. Pole tena, This is Simba broo, ... Taifa Kuuuubwa! Wekundu wa Msimbazi, .... kiakiakiakiaaaaaa

      Delete
  2. mpaka wanachukua ubingwa walikua hawajapotezza...ila wameshindwa kumaliza ligi bila kupoteza.....wewe kilaza hujaelewa nn hapo?????

    ReplyDelete
  3. Bwana wee vipi wasema pesa si sababu ya kiporomoka, ni wazi wachezaji waligoma kwakuwa hawalipwi chao halafu unasema sababu si pesa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic