May 25, 2018


Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, wakiwa wamebakiza mechi moja waweze kukamilisha msimu wa ligi kuu ameibuka na kusema kuwa wachezaji waliomaliza mkataba na mabingwa hao wasiondoke ili wacheze Klabu Bingwa msimu ujao.

Simba ambao ndiyo mabingwa wapya wa msimu wa 2017/18, walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Jumamosi iliyopita ambapo itashiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

Kwa mujibu wa gazeti la ChampioniDjuma alisema kuwa wao wanauachia uongozi kuweza kushughulikia masuala ya mikataba ya wachezaji lakini pia hata wachezaji wenyewe kama wanataka kucheza ligi hiyo, basi waongeze mkataba mwingine katika klabu hiyo.

“Kuhusu wachezaji waliomaliza mikataba yao akiwemo Kichuya hilo tunawachia viongozi washughulikie na hata wachezaji wenyewe ndiyo wana maamuzi ya kubaki au kuondoka, ila wanajua kuwa msimu ujao tunacheza Klabu Bingwa Afrika hivyo ni fursa kwao kushiriki kama wakiondoka basi watakosa nafasi hii muhimu,” alisema Djuma.

Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Kichuya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo.

2 COMMENTS:

  1. Viongozi wa klabu shughulikieni mikataba ya wachezaji wetu haraka. Hatuwezi kumwacha Kichuya kuondoka ana mchango mkubwa sana kwenye ubingwa wetu mwaka huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic