May 25, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji Mtanzania anayecheza soka katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco amerejea Tanzania kwa ajili ya mapumziko baada ya Ligi Kuu nchini humo kumalizika.

Msuva amerejea Tanzania huku timu yake ikimaliza ligi ikiwa imeshika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi nchini humo 'Batola Premier League' ikiwa imejikusanyia alama 48.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kutikisha nyavu mara 11 kwenye ligi hiyo tangu aanze kuitumikia Jadid msimu wa 2017/18.

Msuva atakuwa nchini mpaka mwishoni mwa mwezi Juni kabla ya kurejea tena Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic