May 29, 2018

KOCHA HANS VAN DER PLUIJM AKIMKARIBISHA KUTINYU ALIPOTUA SINGIDA UNITED, WOTE WAWILI WAMETUA AZAM FC.



Mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu ameondoka Singida United na kujiunga na Azam FC.

Taarifa zinaeleza, Kutinyu raia wa Zimbabwe ameamua kumfuaa kocha wake wa zamani, Hans van der Pluijm ambaye ameondoka Singida United na kujiunga na Azam FC.

Mmoja wa viongozi wa Singida United amesema Kutinyu ameondoka na kujiunga na Azam licha ya kwamba alikuwa anawaniwa na Simba.

“Mwisho amekwenda Azam FC, hivyo si Simba tena maana nao walikuwa wakimhitaji,” alisema.

Usajili umeendelea kuunguruma chinichini na kila upande ukipambana kuimarisha vikosi vyao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic