May 4, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuupiga kalenda Mkutano Mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili ya Mei 6 2018.

Hatua hiyo imefikia kutokana na kuingiliana kwa ratiba ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shrikisho Afrika ambapo hivi sasa timu imeweka nguvu zake kwenye michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa viongozi wapo kwenye majukumu na kikosi hivi sasa huku akieleza kuwa utakuwa ni wakati mwafaka kwa Kamati ya Uchaguzi kuanza maandalizi mapema.

Kufuatia kikao kushindwa kufanyika Jumapili ya wiki hii kama ambavyo kilikuwa kimepangwa, sasa kitafanyika June 17 2018.

Jana kikosi cha Yanga kimeondoka nchini kuelekea Algeria tayari kwa mpambano wa mechi ya mkondo wa kwanza katika Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa Mei 6 2018.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic