May 4, 2018



Wakati Yanga wakiondoka nchini jana kuelekea Algeria kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger, inaelezwa kuwa mashushushu wa timu hiyo walikuwa jijini Dar es Salaam kuwafuatilia.

Alger walituma watu maalum waliokuja nchini kuitazama Yanga ilipokuwa inakipiga dhidi ya watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa ligi uliopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa.

Ujio wa watu hao maalum waliokuja kuchunguza mbinu za Yanga, unaweza kuwa faida kwa Waarabu hao ambao watakuwa wenyeji katika mechi hiyo itakayopigwa Mei 6 mjini Algiers.

Tayari kikosi cha Yanga kipo njiani hivi sasa kuelekea Algeria ambapo kitapitia Dubai kabla ya kuwasili nchini humo.


2 COMMENTS:

  1. Kati ya wachezaji walowachwa katika safari hiyo ni Chirwa, Canavaro na Yondani. Naukanushe uwongozi wa yanga

    ReplyDelete
  2. kumbe wameachwa, sio wamegoma kwenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic