MWANACHAMA SIMBA AIBUKA KUPINGA MKUTANO WA KESHO AKIELEZA NI BATILI, ADAI KATIBA IMEFOJIWA
Na George Mganga
Zengwe limeanza tena kuelekea Mkutano Mkuu wa dharura katika klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wanachama wameibuka na kuupinga wakieleza kuwa ni batili.
Felix Makua ni mmoja wa wanachama aliyeibuka na kupinga mkutano huo akidai upo kinyume na katiba ya Simba ambayo haihuruhusu mabadiliko ya katiba.
Akiongea kupitia Radio One, Makua ameeleza kuwa katiba ya Simba inayoenda kupitishwa imefanyiwa uchakachuaji kwa kufojiwa huku akisema mkutano huo hautambuliki.
Mbali na kupinga mkutano, Makua amesema pia katiba ya Simba haihuruhusu kufanya mabiliko yoyote ya kikatiba kupitia mkutano wa dharura na badala yake mkutano mkuu pekee ndiyo huwa unahusika.
Mwanachama huyo ameibuka ikiwa ni siku moja pekee imesalia kuelekea mkutano huo utakaolenga mabadiliko ya katiba yenye madhumuni ya kupitisha rasmi mabadiliko ya kisasa ya uendeshwaji wa klabu hiyo.
Hata hivyo malalamiko hayo yanakuwa kama yanakosa nguvu kutokana na serikali kuyapitisha rasmi japo ikitaka mwekezaji achukue asilimia 49 huku 51 ziende kwa wanachama.
We achana na kuwarusha rusha ni kuwapa kiki. Habari kama hiz angekuwa mnaachanazo
ReplyDeleteHuyo ikiwa alitegemea kuendesha yake kwakuiifukarisha Simba sasa Mheshimiwa Mo keshazifunga njia za wababaishaji na wamekuwa wakibweka ovyo kama wamesomewa albadiri hivo wakatafute kwengine kupata halali yao na hao kwani ninani kwa simba nafukuzwe kwa kipigo cha mbwa koko kinywa juu. Loo wala hawana haya. Hiyo katiba kaiandika yeye?
ReplyDeletewapo wengi hao tegemezi
ReplyDeleteTusimame imara kujenga simba mpyaaa
ReplyDeleteMuda wao ulishapita hao mabwege. Kizazi kipya tupo wengi kuliko wao na haturudi nyuma kwa hatua tuliyofikia. Wakaolewe tu kama hawawezi kununua hisa wakafaidika kwa njia halali. Njaa mbaya sana wallah
ReplyDelete