May 28, 2018


Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, anatarajiwa kusafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu.

Ngoma ambaye alikuwa Yanga alishindwa kuwa sehemu ya kikosi kutokana na majeraha ambayo yalimshika na kusababisha asicheze takribani msimu mzima unaomalizika leo.

Azam FC walifanikiwa kumalizana na kuweza kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wake uliokuwa umesalia.

Mchezaji anatarajiwa kuelekea Afrika Kusini siku yoyote kuanzia leo kufanyiwa vipimo vya afya na baadaye matibabu endapo itabainika inahitajika kufanyiwa hivyo.

1 COMMENTS:

  1. Hongereni sana Azam FC, nakumbuka hata kwa Frank Domayo ambaye baada ya kusajiliwa kutoka Yanga akagundulika kuwa na matatizo, baada ya matibabu sasa ameanza kuonyesha uwezo wake wa kufunga na amefunga mabao muhimu ndani ya timu yetu.
    Lazima timu zihakikishe zinawatibu wachezaji wake ili wawe hazina kwa klabu zao, haina maana kumlipa mshahara mchezaji halafu kila siku unasema majeruhi wameongezeka ndani ya klabu yetu wakati wataalamu wa kuwatibia wapo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic