May 28, 2018


Mtanzania Mbwana Samatta anayecheza soka lake barani Ulaya katika klabu ya KRC Genk, anatarajia kuwasili nchini siku yoyote kuanzia leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki unaowakutanisha marafiki wake na wale wa Msanii Ali Kiba.

Samatta ambaye jana aliisaidia Genk kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, alifunga bao moja mnamo ya dakika ya 18 huku mechi hiyo dhidi ya Zulte Weregem ikimalizika kwa matokeo hayo.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Juni 6 2018 ambao utakuwa na lengo la uchangishaji wa fedha za vifaa vya wanafunzi.

Taarifa zinaeleza mapato ya mchezo huo yatahusika katika ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia wanafunzi ili kuboresha sekta ya elimu nchini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic