May 14, 2018



Na George Mganga

Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, ametupiwa lawama na baadhi ya mashabiki wa soka nchini kufuatia kikosi chake kufungwa mabao 2-1 na Mali.

Ngorongoro wamekubali kichapo hicho katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana ikiwa ni kuelekea kufuzu mashindano ya AFCON (U20).

Baadhi ya mashabiki wameeleza kuwa Ninje amekula jeuri yake kutokana na kutompanga Mlinda Mlango Ramadhani Kabwili na badala yake kumuweka langoni kipa kutoka JKU ya Zanzibar, Peter Mashauri.

Wapo wanoamini kupoteza kwa Ngorongoro jana ni kutokana na kiwango dhaifu cha Mashauri huku wakieleza Kabwili ana uzoefu.

Ninje alimuondoa Kabwili kwenye kikosi hicho siku za hivi karibuni akieleza alichelewa kufika kambini huku Yanga wakimsafirisha kuelekea Algeria kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Licha ya kutemwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rais wake, Wallace Karia, ulimrejesha kikosi Kabwili lakini Ninje hakuweza kumpanga kwenye mechi ya jana.

Matokeo hayo yanailazimu Ngorongoro kushinda mabao 2-0 ili kusonga mbele katika mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Bamako.


3 COMMENTS:

  1. Inashangaza sana baada ya miaka karibu sitini baada ya uhuru ambapo kizazi kikubwa cha sasa cha kitanzania kilikuwa hakija zaliwa lakini cha ajabu athari za kutawaliwa zimeshamiri zaidi miongoni mwa watanzania pengine kuliko hata nyakati za utumwa. Kwa kasumba za kipuuzi na za kimakusudi kabisa Mtanzania wa leo ameidhinisha bila ya utata yakwamba mtu akimudu kuigiza kiengereza katika jamii yetu amehalalika kuwa ni mtaalam na anaweza kukabidhiwa majukumu mazito tu ya kiutendaji. Jamani wachina,wajerumani, wafaransa,warusi wamefika pale walipo kwa kutumia na kuamini lugha zao zilizotumiwa na wataalamu wao wa ndani.

    ReplyDelete
  2. Serious MI sijui kuwateua Hawa makocha night vigezo gani hivi huyu Licha so ndio Ali prove failure Kimberly name challenge jamani why bado tunaye tuu au huwa Sisi hatujifunzi kutokana na makosa or bado tunaimani kuwa loosing winning ni bahati

    ReplyDelete
  3. Huyu kocha hana lolote nilishasema. hivi mtu anachezea club kama YANGA OR SIMBA,AZAM unamaind eti amechelewa kambi. huyo mtu unamfundisha kipi kipya. sasa unampanga mtu mwingine kisa chuki binafsi ona sasa tumefungwa. mbona akina Samatta wanakujaga siku moja kabla ya mechi na mnawapanga. Uko kambini mnafundishaga uchawi au mpira.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic