UONGOZI SIMBA WAELEZA SABABU ZA UJENZI WA UWANJA BUNJU KUSIMAMA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Haji Manara, umeweka wazi kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wao uliopo Bunju, Dar es Salaam, kusimama.
Manara ameeleza kuwa sababu ya mwendelezo wa Uwanja huo kutoendelea ni kutokana sakata la viongzi wao wa juu, Rais wa Simba, Evans Aveva pamoja na Makamu Nyange Kaburu kuwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Radio EFM, Msemaji huyo amesema hayo kutokana na maswali mbalimbali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kutaka kujua ujenzi wa Uwanja huo umefikia wapi.
Ikumbukwe Simba walianza harakati za ujenzi wa Uwanja huo mwaka jana lakini baadaye viongozi hao tajwa juu wa klabu walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo Dar es Salaam kwa makosa ya utakatishaji fedha kiasi cha dola 300,000 ambazo ni sawa na milioni 700 za Kitanzania.
Bado shughuli za ujenzi wa Uwanja wa Bunju umesimama wakati huo klabu ya Simba ikijiandaa kuelekea mkutano mkuu wa mabadiliko ya kikatiba utakaofanyika kesho Jmapili. Pengine ujenzi huo unaweza ukaendelea baada ya klabu kuingia rasmi katika mfumo wa kisasa wa uendeshwaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment