October 2, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kimesepa na pointi tatu mbele ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa leo Oktoba 2.


Bao la ushindi limejazwa kimiani na nyota wao mpya Jesus Moloko ambaye alipachika bao hilo dakika ya 16 kipindi cha kwanza na lilidumu mpaka kipindi cha pili.

Mpaka dakika ya 90 inakamilika bado ngoma ilikuwa Yanga 1-0 Geita Gold jambo lililopeleka furaha kwa mashabiki wa Yanga.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 6 kibindoni na unakuwa ni wa pili mfululizo kwa msimu wa 2021/22. 

Walianza kushinda mbele ya Kagera Sugar ambapo mtupiaji alikuwa ni kiungo wao Feisal Salum ambaye alifunga bao la kwanza kwa Yanga msimu huu.

7 COMMENTS:

  1. Hongera yao, vipi leo kulikuwa hakuna ahadi ya kitita kwa Geita Gold?

    ReplyDelete
  2. Kelele zote zile Bao moja?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuona timu imebadilishwa ili kupata combination inayoendana na wachezaji waliopo? Vibwetere hawaelewagi kitu!

      Delete
  3. Wadhamini wao watakujibu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic