October 1, 2021

 


SHIRIKISHO la Soka Tanzania ‘TFF’ limesema limepokea ripoti ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Septemba 25 huku wadau wengi wakisubiri kuona mlinzi wa Yanga, Yanick Bangala atakutana na rungu gani.


Bangala alionekana akionyesha ishara isiyokuwa ya kiungwana dakika ya 59 ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.


Kupitia ripoti iliyokabidhiwa na mwamuzi Kayoko, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), inaweza kumtia hatiani Bangala kwa mujibu wa kanuni ya 39 ibara ya 5 ya udhibiti wa wachezaji ambapo anaweza kufungiwa michezo mitatu na faini isiyopungua Sh 500,000.


Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema: “Baada ya mchezo wa Jumamosi wa Simba dhidi ya Yanga, mwamuzi Ramadhani Kayoko aliwasilisha ripoti ya mchezo huo kwa kamati zinazohusika, na kupitia mwenendo wa mchezo kama kanuni inavyomtaka kufanya hivyo ndani ya saa 24.

“Hivyo kuhusu hilo tukio la mchezaji wa Yanga na changamoto zote za kinidhamu ambazo zilitokea kwenye mchezo huo, na baada ya kupitiwa ripoti hiyo tunatarajia kutoa taarifa ya maamuzi hivi karibuni.”

8 COMMENTS:

  1. Ni upuuzi tu tff mnakwama kuendesha Mpira na marefa wenu mechi ya simba na biashara rafu mbaya ya wazi TV imeonesha refa kaona kabisa hakutoa adhabu ya kadi nyekundu dangerous play ila mechi ya Dodoma jiji refa hakuona mpaka kaambiwa na wachezaji wa simba ndo Katoa kadi hii kwakweli mnafeli Sana. Ujinga mtupu

    ReplyDelete
  2. Tff tunaomb muongez ufanisi juu ya usimamiz wa sheila na kanuni za kimichezo ikiwa n kuchukua hatua kwa haraka zaiid

    ReplyDelete
  3. Siku hizi ni kazi kutofautisha Waandishi wa habari za michezo na waandishi wa habari za udaku. Yaan hilo la Bangala ndo tukio pekee kwenye huo mchezo kiasi cha mwandishi kwenda TFF kuulizia kama nalo liliwekwa kwenye ripoti au la? Mnakosa weledi sana

    ReplyDelete
  4. Tff na Simba ni watoto wa mtu mtu mmoja hawana jipya

    ReplyDelete
  5. Sheria ichukue mkondo wake, TFF tunawaomb pia mlitazame vyema hili tatizo la baadh ya timu kutotumia milango inayokubalika, nahc adhabu iongezwe kwa timu inayorudiarudia. Msisahau kulifatilia suala la timu znazocheza na simba kuahid mil15, linaharufu ya RUSHWA na UBADHIRIFU WA PUBLIC FUND

    ReplyDelete
  6. Natarajia kuona adhabu Kali dhidi ya muamuzi wa pembeni aliekataa goli la pili la yanga lililofungwa na fectoni mayele kwa kigezo Cha mchezadi kuzidi kitu ambacho sio kweli tizameni vizuri viongozi tff ili kuweka mzani sawa wa hukumu msiwatolee macho wachezaji tu mana mmeshaanza kwa bangala mnataka kuanza kuitenza nguvu yanga ili timuzenu zifanye vizuri fanyeni kazi acheni ushabiki mnatuharibia mpira

    ReplyDelete
  7. Moira wabongo tff ndowana ualibu2

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic