May 7, 2018

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekubali mpango wa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kutoka Manchester United kuelekea Juventus msimu huu wa joto (Tuttosport, via Daily Express)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kuwa na matamanio ya mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele,aliyejiunga na mabingwa wa Ulaya na Uhispania, Barcelona( Catalan giants) kwa kitita cha £135m msimu uliopita, iwapo kiungo huyo mwenye wa umri wa miaka 20 atapatikana. (Sun)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic amesisitiza kwamba Manchester United haina makubaliano yoyote ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa kutoka Serbia. (Manchester Evening News)
Liverpool imepinga ripoti kutoka Ufaransa kwamba ilikuwa imekubali mkataba wa kumsajili nahodha wa Lyon Nabil Fekir. (Liverpool Echo)
Meneja anayeiaga Arsenal Arsene Wenger ameonekana akiombwa tai yake na shabiki mchanga katika mechi ya fainali ya nyumbani na alikubali bila pingamizi yoyote. (London Evening Standard)
Kutoka BBC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic