May 11, 2018


Licha ya kueleza kuwa imeyumba kiuchumi, klabu ya Yanga ipo katika mchakato wa kushusha mshambuliaji Mtogo, Djako Arafat, kutoka Welayta Dicha SC.

Taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zinaeleza kuwa klabu hiyo inatarajiwa kumleta mshambuliaji huyo kuja kuimarisha safu ya ushambuliaji iliyo na mapungufu.

Yanga inamleta Djako kwa ajili ya kusaidia Yanga inayoshiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ujio wa Djako unatajwa kama mbadala wa Donald Ngoma ambaye amekosekana dimbani kwa muda mrefu zaidi kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Taarifa za ujio wa mshabuliaji huyu zimezidi kushika kasi ikiwa inajiandaa na mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda utakaopigwa Mei 16 2018.

2 COMMENTS:

  1. Hawana Ubavu wa kumleta huyo mchezaji hata kwa dawa...Kama tunabisha pinga ila haya ni maneno ya kuuza magazeti

    ReplyDelete
  2. Kwanini Yanga wazidi kujilimbikizia madeni wakati wachezaji waliokuwepo wanashindwa kuwahudumia? Kila mtu anajua chanzo cha matatizo yanayoikabili Yanga hivi sasa ni kule kutaka kushindana na Simba wakati ule wa usajili. Wahenga wamesema ari bila ya mali ni masuala ya kutafuta muhali na dunia na ndicho kinachoitafuna yanaga hivi sasa na bado.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic