May 30, 2018


Baada ya kuelezwa kwa baadhi ya wachezaji Yanga kuwa wanaondoka ndani ya klabu hiyo kutimkia mahala pengine, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ameeleza kuwa hawawezi kuruhusu mchezaji mwingine aondoke zaidi ya Ngoma.

Nyika amepiga mkwara huo kutokana na taarifa mbalimbali kuripotiwa kuwa wachezaji wao wengi wanaweza kuondoka ikiwa dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa bado wachezaji wote wapo pamoja na Yanga, na endapo ikitokea wakaondoka labda uongozi wenyewe uamue wafanya hivyo.

Ikumbukwe mpaka sasa Yanga imesharuhusu Ngoma kutimkia Azam FC huku baadhi ya wachezaji wake wengine wakielezwa kutaka kuihama timu hiyo.

Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Andrew Vincent na Juma Abdul ni miongoni mwa wachezaji walio katika tetesi zinazohusishwa kutimkia Simba au Azam FC.


2 COMMENTS:

  1. Huwezi kumzuia binadamu kwenda kutafuta maisha bora anapotaka kwenda. Kama kiongozi unachopaswa kufanya ni kuwaboreshea vipato vyao wachezaji ili wasiondoke, lakini kama viongozi hamtawalipa mishahara yao wachezaji hivi nguvu ya kumzuia mchezaji huyo unaitoa wapi? Tuwe wakweli na tutende haki.

    ReplyDelete
  2. Kutokana shok walioyoipata ya kukimbiwa na nyota, yanga haijuwi inafanya nini. Vipi watawazuia wachezaji kuondoka wakati sheria inaruhusu kutokana na kumalizika kwa mikataba yao na huku ngoma wao wenyewe wameshatamka kuwa wameshamfuta katika kikosi cha yanga. Kwa kutamka kuwa hawataruhusu mchezaji kuondoka baada ya Ngoma. Sharia gani inayowaruhu yanga kuwazuia?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic