June 1, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya KMC iliyopanda daraja kutoka Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imemtangaza Mrundi, Etienne Ndayiragije, kuwa kocha wao mpya kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili.

Ndayiragije aliyekuwa akiifundisha Mbao FC ametia kandarasi ya miaka miwili na KMC tayari kwa kuanza kuiandaa kuelekea msimu mpya ujao wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Mrundi huyo ametua KMC kuchukua nafasi ya Mzawa, Fredrick Minziro aliyeipandisha daraja timu hiyo kucheza ligi kuu.

Mbali na kuipandisha KMC, Minziro pia aliwahi kuipandisha daraja klabu ya Singida United ya mjini Singidana baadaye kuachwa kisha Mholanzi, Hans van der Pluijm kupewa timu hiyo.

Awali Ndayiragije alikuwa anahusishwa kusajiliwa na Singida United ili kuchukua nafasi ya Pluijm aliyetimkia Azam FC lakini KMC wamemuwahi kwa kuingia naye mkataba wa miaka miwili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic