June 1, 2018

Klabu ya Chelsea ya Uingereza itajaribu kumshawishi aliyekuwa mkufunzi wa Real Madrid aliyetangaza anaachia ngazi Zinedine Zidane kuwa mkufunzi wake mpya (Sun).
Matumaini ya klabu ya Manchester United ya kumsajili Gareth Bale, 28, huenda yakafifia huku mchezaji huyo wa taifa la Wales akitarajiwa kusalia kufuatia kuondoka kwa Zidane. (Daily Mirror)
Real Madrid huenda ikamnyatia mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino - ambaye alitia saini mkataba mpya wa miaka mitano na timu yake wiki iliopita- ili kuchukua mahala pake Zinedine Zidane aliyeondoka. (Daily Mirror)
Lakini Real pia inamtaka kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, amaye aliiongoza The Reds kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya. (Sun)
Kandarasi ya Pochettino katika klabu ya Spurs haina kipengee ambacho kinaweza kumruhusu kuondoka na mwenyekiti wake Daniel Levy yuko tayari kuhakikisha kuwa anasalia katika klabu hiyo.(Daily Telegraph)
The Blues pia huenda wakamlenga mkufunzi wa Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc kuchukua mahala pake Antonio Conte. (Daily Mail)
Chelsea inasema kuwa haitalipa dau la £7m ili kununua kandarasi ya mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri. (Guardian)
Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic