June 1, 2018





Mshambuliaji Mohammed Rashid anatarajia kuanza kuichezea Simba katika michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza keshokutwa mjini Nakuru, Kenya.

Mohammed amejiunga na Simba akitokea Prisons na taarifa zinaeleza kwamba amemalizana na Simba jana usiku.

“Kweli wamemalizana na yeye sasa ni safari ya kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya SportsPesa,” kilieleza chanzo.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo alikataa kuongeza mkataba na Prisons ingawa hakuwa amesema anataka kufanya nini.

Taarifa zinaeleza alikataa kuongeza mkataba mpya baada ya kukubaliana jambo na Simba, hivyo alikuwa akisubiri kumalizika kwa msimu.

5 COMMENTS:

  1. Maamuzi mazuri yaliyofuata taratibu za mpira. Lakini nilisikia wachezaji wageni hawataruhusiwa kucheza kwenye mashindano hayo, kama ni kweli basi kuna kasoro katika kufikiri. Tatizo ninini kuwakataza wachezaji wageni? Ligi zao zimekwisha wamejiunga na timu mpya, kosa lipo wapi? Viongozi nipeni ufafanuzi.

    ReplyDelete
  2. Anaejuwa ningependa atujuilishe sababu ya kutoshiriki idadi ya nyota wa Simba safari ya Kenya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic