BAADA YA KASEJA, MWINGINE KUTOKA MBAO AUNGANA NA NDAYIRAGIJE KMC
Baada ya kipa mkongwe na mwenye heshima ya kipekee Tanzania, Juma K Juma, kujiunga na KMC kwa kusaini mkataba wa mwaka, mchezaji mwingine aliyekuwa chini ya Kocha Etienne Ndayiragije imeelezwa ametua Mbao.
Yusuph Ndikumana aliyekuwa anaitumikia Mbao FC chini ya Kocha huyo Mrundi wakati huo akiifundisha Mbao inaelezwa tayari ameshamalizana na viongozi wa juu wa KMC.
Taarifa za ndani kutoka KMC zinasema mchezaji huyo amekuwa pendekezo la Ndayiragije kutokana na mchango wake mkubwa ambao aliouonesha wakati akiicheza Mbao.
KMC ambayo ilipanda daraja kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao imeendeleza mipango yake mathubuti ya kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuhimili mikiki-mikiki ya ligi.
Jumla ua timu 20 zitashiriki ligi msimu ujao tofauti na ilivyokuwa mwanzo na itakuwa mara ya kwanza kwa ligi ya Tanzania kuwa na idadi ya timu hizo.








0 COMMENTS:
Post a Comment