June 24, 2018


Michuano ya Kombe la Dunia Urusi inazidi kuwaka moto ambapo leo timu moja kutoka Afrika ambayo ni Senegal itakuwa kibarua dhidi ya Japan.

Senegela inaingia Uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Poland kwenye mchezo uliopita.

Nahodha wa kikosi hicho, Sadio Mane anapewa nafasi kubwa ya kuwaongoza wenzake kuhakikisha timu hiyo inafuzu kuelekea hatua inayofuata katika kundi H.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 12 jioni na ikipigwa katika Uwanja wa Ekarinburg.

Mechi zingine zinazopigwa leo ni England dhidi ya Panama itakayoanza majira ya saa 9 mchana na nyingine ni Poland dhidi ya Colombia kuanzia saa 3 usiku.

1 COMMENTS:

  1. Kila la kheri Senegal ila lazima kama Taifa huru lenye watu karibu million 60 vipi tunashindwa angalau kukaribia kushiriki kombe la Dunia?
    Kitu kimoja mpaka sasa mimi bianafsi nilichojifunza kwenye mashindano haya ya kombe la Dunia ni kwamba mpira ni kocha bwana. Timu zile za warabu zina wachezaji wazuri tu lakini kilichowaangusha ni makocha wao ni wa viwango vya chini wanakosa mbinu za kisasa za ufundishaji wa soka. Wale warabu wanaotututemesha sisi tunapokutana nao kama vile swala anapokabiliana na Simba wenzetu wamewatumbua kama nyanya iliooza. Nafikiri wadau wa mpira nchini wangeunda jopo la wataalamu kwenye haya mashindano ya kombe la Dunia kuzifanyia ujajusi wa hali ya juu kubaini madhaifu yao ili tunapokutana nao isiwe kikwazo tena kwami wametunyanyasa vya kutosha. Nakama viongozi wetu wa soka nchini wangekuwa wanafanya kazi ya kwa uweledi inavyotakikana basi wangefanya biga ua kumuajiri kocha wa timu ya Taifa ili ashiriki kikamilifu katika kuyafanyiya tasmini mahsusi mashindano haya ya kombe la Dunia kwa manufaa ya Timu ya Taifa. Mimi sina imani na uongozi wa TFF hata kidogo kwa sababu sioni jipya wanalolifanya isipokuwa kuwachukia wanaowakosoa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic