June 7, 2018


Uongozi wa klabu ya Singida United umesema kuwa hautakuwa na mchezaji wake msimu ujao, kiungo, Deus Kaseke.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa Kaseke amepata timu ya kuchezea Afrika Kusini hivyo hatokuwa sehemu ya kikosi chao.

Sanga hajaweka wazi jina la timu ambayo Kaseke ataenda kuichezea hivyo hataweza tena kuwepo katika klabu hiyo baada ya mashindano ya Super Cup huko Kenya.

Taarifa hizo zimekuja wakati kikosi hicho kikiwa kinajiandaa kucheza na Gor Mahia FC katika mashindano hayo kwenye hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV