June 15, 2018


Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limekubali maombi ya Yanga kujiondoa katika mashindano ya KAGAME baada ya kutuma barua iliyoeleza kuomba kujitoa

Yanga ilituma barua kupitia TFF ikiomba kujiondoa ili kuwapa nafasi wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Barua hiyo ilieleza kuwa ratiba ya michuano imekuwa si rafiki kwao na itakuwa inawabana sababu wanapaswa kuwajibika kwenye mashindano ya shirikisho pia wachezaji wake wengi hawana mikataba.

Kutokana na maombi hayo, CECAFA wamemua kuuwaalika Vipers SC ya Uganda kuchukua nafasi ya Yanga ambapo katika kundi C wataungana na Simba, Dakadaha ya Somalia na St. George ya Ethiopia.

Michuano hiyo inatarajia kuanza kurindima June 28 mwaka huu na kumalizika Julai 13 2018.

6 COMMENTS:

  1. Ohooo nafasi ya Yanga inazibwa na timu ya nchi nyingine? Tunapoteza nafasi ya Tanzania. Kihalali ingechaguliwa timu nyingine kutoka Tanzania sio Uganda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii ndio CECAFA ya Musonye ata Tanzania kupewa nafasi 3 ni kuangalia malaise zaidi

      Delete
  2. Inaonekana TFF ni kiini macho, haina kauri kwa CECAFA. Kama Tanzania ilitakiwa kuingiza timu tatu, then kwanini isingechaguliwa timu kutoka Tanzania!? Au Yanga ilikuwa inang'ang'aniwa kwa ajili ya maslahi tu!?

    ReplyDelete
  3. MasQeeen yangaaa. Walidhani Dunia itasimama wakiukimbia Taïga kubwa,������.

    ReplyDelete
  4. Hapo ndo utajua kwanini Yanga ilipangwa na Simba kundi moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic