STAA anayependwa na mashabiki wa Simba kutokana na uwezo wake wa kuzinyanyasa timu pinzani, Shiza Kichuya amegoma kuchukua Sh70milioni alizowekewa mezani ili aongeze mkataba mpya.
Kichuya ni kati ya wachezaji wa Simba ambao mikataba yao imemalizika msimu huu wa Ligi Kuu Bara akiwemo Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo. Wakati Simba wakiendelea na mazungumzo ya kumuongezea mkataba Kichuya, Azam FC nayo
imeelezwa kuingia vitani ikitaka kumsajili kiungo huyo anayetumia mguu wa kushoto.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi imezipata zinasema, kiungo huyo akiwa na meneja wake, uongozi wa Simba walishindwa kufikia muafaka mzuri wa kumuongezea mkataba mpya kiungo huyo kutokana na dau kubwa analolitaka.
“Uongozi wa Simba bado unapambania jinsi ya kumsainisha Kichuya na hakuna kingine zaidi ya fedha pekee ambayo ndiyo imekwamisha kwani kuhusu mazungumzo ya awali tayari yamefanyika na mwenyewe ameonyesha nia ya kuongeza mkataba.
“Kama Kichuya akipatiwa fedha anayoihitaji tofauti ya shilingi milioni 70 aliyoikataa basi ata
saini mkataba, lakini tunashukuru mazungumzo yetu Simba na yeye mchezaji yanakwenda vizuri,” alisema mtoa taarifa huyo. Kaimu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ jana alizungumzia usajili wa Kichuya na kusema kuwa: “Wachezaji wetu wanne tupo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya kuongeza mkataba mwingine mpya, akiwemo Kichuya.” “Kichuya tupo kwenye mazungumzo naye mazuri ambayo tutayafikia muafaka hivi karibuni kwani yeye mwenyewe na meneja wake tulikutana na kujadiliana nao.
“Mchezaji huyo bado tunamuhitaji katika timu yetu kutokana
na mchango mkubwa alioutoa kwenye msimu huu wa ligi na kutuwezesha kutwaa ubingwa wa ligi,” alisema Abdallah.
“Hakuna mchezaji tunayemuhitaji tukashindwa kumsajili, kama uongozi tumepanga kumsajili mchezaji yeyote tutakayemuhitaji kutokana na mapendekezo ya kocha atakayoyatoa,” alimalizia Abdallah ambaye si mzungumzaji sana kwenye vyombo vya habari. Baba wa Kichuya alinukuliwa na Championi akimtaka mwanae asisaini mkataba kwa mazoea Simba bali aangalie masilahi yake na soko lake.
Mfano kichuya apewe millioni mia moja 100 na Azam halafu asaini Azam kwa malengo gani hasa? Azam haishiriki mashindano yeyote ya kimataifa yatakayo mpa kichuya nafasi ya kujitangaza zaidi. Hii itakuwa sasa ni sawa na hadithi ya bwana mwenye kuku aliekuwa akimtagia yai la dhahabu kila siku lakini kwa tamaa jamaa akaona isiwe shida ni bora kumchinja kuku ili kuchota dhahabu yote iliyomo ndani ya kuku lakini matokeo yake anapoteza kuku na dhahabu. Nadhani kama ningelikuwemo kwenye timu ya uongozi wa Kichuya inayomuongoza katika masuala ya mikataba na maisha yake ya soka basi ningechukuwa milioni 50 za Simba kwa sasa na kuziacha milioni mia mbili 200milioni za Azam. Ndio au labda kama Kichuya amesharidhika kumalizia soka lake Tanzania. Nadhani malengo kwa vijana wetu hasa wale wenye vipaji ni kuifikiria mikataba ya akina Sadio Mane, Victor wanyama, Samata nakadhalika. Amini katika Dunia hii kwa bidii Mungu kamwe haachi kumuunga mkono menye kujibidiisha na hakuna kisicowezekana.
ReplyDeleteMashindano ya Kimataifa yenyewe Timu inacheza Mechi 2 Tu imetolewa. Kichuya aangalie Maslahi Mapana. Kama ataweza Kukuza Kipaji chake Ataonekana tu hata akiwa AZAM FC na Timu ya Taifa...
DeletePiga ua haendi Azam wala Yanga...mtabaki macho kodo
DeleteKwani simba ilipomsaini niyonzima kwa mil 150 mwaka Jana wamefika wapi?
ReplyDeleteHaya Mkwasa jitutumuwe mbona kimya nanyi si mnamtaka mbona kimya?
ReplyDeleteWanajidanganya tuu, hivi Kichuya aende Aam au Yanga wakati huu wakati yeye kapigania ubingwa wa Simba na sasa ni mabingwa, hivi inawezekanaje? Kichuya atabakia Simba hata kama kumkopa Simba ikubali deni lakini ni kweli Kichuya anastahili zaidi ya Sh 70m. Amecheza mechi zote za Ligi, na ameassist goli 28, mbali ya yeye kufunga magoli na ni mpambanaji uwanjani muda wote. Anastahili kulipwa zaidi.
DeleteNakumbuka Mbwana Sammata alicheza mechi kama mbili za klabu bingwa Afrika, na Leo yuko huko duniani, kwa hiyo idadi ya mechi sio shida, shida ni kiwanja gani na ni mashindano gani
ReplyDeleteSahihi kabisa Mic mambo haya sana inategemea na timu unayokutana nayo, aina ya mashindano na uwanja bana. Mbwana Samatta pengine bila hivyo asingelionekana kipindi kile pengine angeonekana umri umeshakwenda.
Delete