June 7, 2018


Na George Mganga

Singida United imeshindwa kufuzu kucheza fainali ya Super Cup nchini Kenya kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Gor Mahia FC kwa mabao 2-0.

Meddie Kagere amekuwa shujaa wa mchezo huo kwa kufunga mabao yote mawili na kuiwezesha Gor Mahia kutinga hatua ya fainali.

Baada ya ushindi huo, Gor Mahia imeungana na Simba kucheza fainali itakayopigwa Jumapili ya wiki hii.

Simba ilikuwa ya kwanza kufika fainali kwa ushindi wa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kwenda suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC.

3 COMMENTS:

  1. Singida haijaaga bado itacheza kutafuta mshindi wa TATU

    ReplyDelete
  2. Simba wanatakiwa kuwa makini katika masuala ya hujuma kuelekea mchezo wa fainal kwani wakenya si watu wazuri katika masusla ya fitna na inaonekana kwa vyovyote vile piga ua wamedhamiria kupeleka timu Uingereza.

    ReplyDelete
  3. Kabisa, hata leo kulikuwa na viishara hivyo dhidi ya Singida

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV