June 7, 2018






Nyota wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Ally Saleh Kiba  ‘Alikiba’ amemuonya  mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta kwa kumwambia kuwa atahakikisha timu yake inafanya vizuri watakapokutana kesho Jumamosi katika mchezo maalum wa kuchangia elimu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.


Kesho Jumamosi, timu ya Alikiba na timu ya Samatta, zitapambana kwenye uwanja huo ukiwa ni mchezo maalum wa kuchangia elimu ulidhaminiwa na Kampuni ya Asas.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana, Alikiba alisema kuwa atahakikisha mpinzani wake anaondoka akiwa analia kutokana na kuchagua kikosi bora kwa ajili ya mchezo huo utakaowajumuisha wachezaji wengi wa kimataifa.


“Nitahakikisha Samatta anaondoka analia kwani kikosi changu kipo vizuri nikiwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya Tanzania, tunaye Uhuru Selemani ambaye naamini kwa ushirikiano wake na wengine tutapata matokeo mazuri.

"Lengo la mchezo huu ni kusaidia elimu na tumelenga zaidi shule za msingi, hivyo moja kwa moja fedha zitakazopatikana kwanza nitaangalia shule niliyosoma, halafu Shule ya Msingi Upanga, baada ya hapo tutaangalia wapi tena kuna mahitaji.

“Samatta naye ataanzia kwenye shule aliyosoma, lakini pia tutahakikisha mandhari ya shule nyingi za msingi hapa nchini yanakuwa mazuri kupitia fedha zitakazopatikana, hili tunalolifanya litakuwa mara mbili kwa mwaka, baada ya kucheza hapa Dar, tutaenda tena Mwanza kufanya jambo kama hili,” alisema Alikiba.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic