June 23, 2018


KIUNGO mchezeshaji wa Simba anayesifika kwa mashuti ya mbali, Mohamed Ibrahim ‘Mo Ibra’ rasmi anasaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa dau la Sh. milioni 30 na kuachana na Yanga iliyokwisha muonyesha mkataba wa awali.


MO ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusajiliwa na timu hiyo katika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na walishakubaliana mambo mengi kabla ya Simba kupindua meza kibabe.

Yanga ilitaka kumsajili huyo baada ya kupata taarifa za mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu uliomalizika wa ligi akiwa pamoja na Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin ambao tayari wameongezewa mikataba.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi, kiungo huyo amekubali kusaini kwa dau hilo la usajili baada ya kufikia muafaka mzuri na uongozi wa timu hiyo akitokea Morogoro kwa Basi.

Mtoa taarifa huyo ambaye Championi limejiridhisha 
 naye alisema, MO atasaini kwa dau hilo la usajili kwa mkataba wa miaka miwili huku akiboreshewa mshahara wake wa kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili ambacho atakachokuwepo Msimbazi.

“MO usajili wake umeshakamilika na kilichobaki ni yeye kuja kusaini mkataba pekee, kwani kila kitu tumekubaliana kwa maana ya dau la usajili na mshahara wake wa kila mwezi.


“Na tumekubaliana kwa pamoja kuwa atasaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 30 baada ya kufikia muafaka mzuri kati yetu viongozi na yeye mwenyewe mchezaji.

“Hivyo, MO hatakwenda tena Yanga kama ilivyokuwa inaelezwa na badala yake atabaki kuendelea kuichezea 
 Simba kwa miaka mingine miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa MO ambaye aliwahi kuzinguana na Kocha Pierre Lechantre aliyetimuliwa na Simba, alisema kuwa “Mkataba ni siri kati yangu mchezaji na viongozi, hivyo ni ngumu kwangu kuzungumzia makubaliano yaliyokuwepo katika mkataba wangu.”


“Ni kweli viongozi wananisubiria mimi pekee kusaini mkataba ambao ninatarajia kusaini leo (jana) baada ya kukutana na viongozi kama unavyofahamu nilikuwa safarini,” alisema MO.

10 COMMENTS:

  1. Kuna suala la kupigania maslahi kwa mchezaji ambalo ni jambo muhimu lakini muhimu cha kuzingatia kwa vijana wetu wa kitanzania ni suala la kupigania viwango vyao kuwa bora zaidi. Maslahi bora na mikataba ya thamani huboreshwa na mchezaji mwenyewe na sio muajiri kwa uwezo wa mchezaji,bidii na nidhamu ya mchezaji uwanjani na hata kwenye mazoezi ni moja ya mambo yanayompandisha thamani mchezaji na wala sio kwa mchezaji kubweteka kwa kutegemea kuwa kuna timu nyengine zitakuja kumsajili.

    ReplyDelete
  2. Huu uandishi gani!!!mkiitwa waandishi makanjanja mnatoa povu,eti kiungo Yanga asaini Simba!!!lini huyu mchezaji alikuwa Yanga hadi uandike habari yako na kuipa heading ya namna hiyo...ukosefu wa weledi wa taaluma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi huyu mwandishi namwona kama mwendawazimu.

      Delete
  3. Habari zako zinakosa mvuto jipange kaka

    ReplyDelete
  4. Sasa Mo ni kiungo wa Yanga? Nimeacha rasmi kununua gazeti lenu. Tena na hivyo mmepandisha bei. Bye bye.

    ReplyDelete
  5. Toka nilivyojua wewe ndio mhariri wa Chanpioni niliacha kununua hilo gazeti. Sasa hizi no habari gani!? Lini huyu mchezaji akawa wa yanga!? After all hata hayo mazungumzo ya Yanga na hao wachezaji ni wewe tu na gazeti lako la udaku mlioandika. Hayajawahi kuwepo zaidi ya nyie kutaka kuuza habari.

    ReplyDelete
  6. Kwenye ili kaka umechemsha eb jaribu...kuwa.makini wakati wa kucreate kichwa cha habari...kwa hali hii utafanya watu waache kusoma habari zako...nazani ili utalifanyia kazi...by the way hongera kwa kuteka tention za watu kwenye hii habari������

    ReplyDelete
  7. saleh mnajisahau,wanunuzi wa magazeti yenu ni watu wenye weledi,kwa mfumo huu.mmeharibu biasha yenu.

    ReplyDelete
  8. saleh mnajisahau,wanunuzi wa magazeti yenu ni watu wenye weledi,kwa mfumo huu.mmeharibu biasha yenu.

    ReplyDelete
  9. Kwani MO ni kiungo wa yanga, acheni kudanganya wasomaji wenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic