June 23, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Stand United ya mjini Shinyanga imetajwa kuwa moja ya wachelewashaji sugu wa kulipa mishahara kwa wachezaji wao wanaoitumikia timu hiyo.

Beki wa timu hiyo, Ally Ally, amesema kuwa viongozi wa klabu hiyo wamekuwa wachelewashi wakubwa wa kuwalipa mishahara yao na inafikia wakati wanashindwa mpaka kupokea simu.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha michezo (Spoti Leo), Ally ameeleza kuwa Stand wamekuwa na utaratibu huo wa muda mrefu huku wakishindwa kujua nafasi ya mchezaji ndani ya timu.

Beki huyo ameeleza zaidi inafikia mchezaji anaweza akawa anadai takribani mshahara wa miezi mitatu mpaka minne bila kulipwa na akishaanza kudai anaonekana kuwa msumbufu.

Ally ameweka wazi kuwa bado ana mkataba na Stand na itafikia hatua anaweza akaondoka kuelekea mahala pengine kwa maana ya kushindwa kulipwa mshahara wake ambao anaidai klabu hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa Stand United, Kennedy Nyange, alipotafutwa, ameibuka na kukanusha suala hilo akisema ni propaganda pekee zinazofanywa na Waandishi wa Habari kwasababu kipindi hiki ni cha usajili.

Nyange amewatupia lawama waandishi akieleza kwa sasa wanajaribu kuwaharibia wachezaji ili waondoka na kuelekea katika timu zingine na akisisitiza kuwa hakuna mchezaji anayeidai klabu.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic