June 14, 2018


Na Haji S Manara

Mwenyezi Mungu kila uumbaji ni matakwa yake, sipendi kabisa mnavyowanyanyapaa Maalbino. Ninyanyapaeni mimi kwa niaba yao, nipo tayari sababu mimi nina moyo jasiri.

Sioni hiyo shida, kimsingi mimi siijui tofauti ya wewe unaenyanyapaa na mimi, sanasana nimekuzidi kila kitu.

Naishi pazuri kuliko wewe, natembelea gari zuri kuliko wewe, mimi Maarufu Kati ya watanzania maarufu nchi hii na nina mke na watoto wazuri kukuzidi mara milioni

Hivyo nitutukaneni mimi kwa niaba ya Maalbino wote nimekomaa kifkra kuliko chuma kwa maana kidogo tu wewe albino, kwahiyo maana yake nini.

Halafu mademu zenu wanakuja DM 'Instagram' kutaka namba, ndiyo ninajivunia Muumba alivyoniumba na msijisikie vbaya maalbino, niigeni mimi kuweni Majasiri.

3 COMMENTS:

 1. HII BLOG INAPASWA KUFUNGIWA KABISA MAANA WAANDISHI WAKE SIO WELEDI KABISA KAZI SHOBO NA HABARI ZA YANGA, WAKATI UANDISHI UNAWASHINDA, KICHWA CHA HABARI YAKO UNAANDIKA "WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI" wale ni watu wenye UALBINO sio ulemavu wa ngozi , hebu nioneshe ngozi zao zina ulemavu wapi, ni upungufu wa melanin pigment tu, kwahiyo ukome kuandika watu wenye ulemavu wa ngozi na kuanzia leo andik watu wenye ualbino....fatilia BAKITA kwa ufafanuzi zaidi

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ndiyo, huo ulemavu. Tatizo la mashabiki Wa Yanga mmevurugwa na mnamtukana kila MTU.

   Delete
  2. Kweli nimeamini wewe ni shabiki wa TUNDU SC. na nafaham wiki iliyopita ulikufa 2 nil Kenya na GOR MAHIA, sasa huwenda umelewa supu ya mkia waliokubakishia wenzako, UKWELI NI HIVI NENO ALBINO (NI NENO FASAHA LA KISWAHILI) kweli zaman watu walizoea kuwaita watu wenye ulemavu wa ngozi lakini toka mwaka 2016 BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA(BAKITA), LILIONA HUO NI UNYANYASAJI NA NDIO MAANA WAKAONDOA MATUMIZI YA NENO ULEMAVU WA NGOZI NA KUWATAMBUA WATU WENYE UALIBINO, ANGALIA HATA MANENO YA HAJI MANARA MSEMAJI WA TUNDU SC, KAMA NI KWELI AMEYAZUNGUMZA HAYO MANENO WAPI UMEONA AKISEMA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI, YEYE MWENYEWE AMESEMA MAALBINO KWA KUWA NDIO NENO FASAHA LINALOTAMBULIKA, NADHANI UMEELEWA, NA KABLA YA KUCOMMENT ILITAKIWA UFANYE RESEARCH JUU YA HAYA YALIYOANDIKWA...

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV