Mambo yanazidi kwenda mlama na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kinazidi kudidimia kwenda katika wimbi la u-yatima.
Maana sasa Makamu wa Rais wa ZFA Pemba, Ali Mohammed Ali, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo.
Makamu huyo ameungana na Rais wa chama hicho, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais Unguja, Mzee Zamu Ali na Abdul Ghani Msoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, makamu huyo alisema hatua hiyo imekuja baada ya kujitathimini kwa kina na kuona tayari viongozi wenzake wameshaachia ngazi nyadhifa zao.
“Baada ya kuona viongozi wenzangu wa juu wamejiuzulu nyadhifa zao, sina budi na mimi kujiuzulu kama walivyofanya wenzangu, kuanzia leo tarehe 13/6/2018,” alisema.
Ingawa wamekuwa hawataki kuweka wazi mengi, lakini inaelezwa suala la kikosi cha Zanzibar cha vijana kupeleka wachezaji wenye umri mkubwa katika michuano ya Cecafa, kimekuwa chanzo kikubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment