June 24, 2018


Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kitendo cha yeye kuingia na taulo uwanjani siyo uchawi wala ubishoo bali huwa anakuwa na kazi nalo maalum.

Hivi karibuni Manula aliingia kwenye sintofahamu kwenye michuano ya SportPesa iliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya kutokana na kuingia na taulo uwanjani hali iliyowafanya waamuzi na wachezaji waliondoe huku yeye akionekana kujitetea.

Manula ambaye ni mzaliwa wa Morogoro, amesema kuwa amekuwa akiingia na taulo kutokana na glovu ambazo amekuwa akizitumia zipo za aina mbili, ya kwanza inashika mpira ikiwa na hali ya ukavu na nyingine inashika mpira ikiwa na hali ya unyevu na nyingine kwani nyingi zimekuwa zikitunza unyevunyevu hali inayomlazimu kuingia nalo uwanjani.

Kipa huyo ambaye mshahara wake wa kwanza kwenye soka ulikuwa 150,000 alisema kukaa na taulo golini kwake inamsaidia kujifutia pindi inapotokea jezi na gloves zimelowa na siyo ubishoo kama wengi wanavyosema bali yeye ni mshamba.

“Taulo inanisaidia inapotokea siku nimetumia gloves isiyohitaji maji na jezi zinakuwa zimelowa hivyo inasaidia kujifutia na ni ngumu kujifutia kwenye jezi, kwa hiyo siyo ubishoo mie ni mshamba wa mbali napenda sana mihogo, nikiona madafu natamani kwani nyumbani kwetu minazi ipo mingi.

 “Taulo haliwezi kuleta kitu chochote cha ajabu, kwenye mechi na Gor Mahia nilikuwa nalo na tukafungwa. Ujue mtu kuhusisha kitu fulani siyo dhambi kwa sababu ni yeye kwa muono wake na mtazamo wake lakini mimi ninayetumia taulo nimeshasema sababu za kulitumia,” alisema Manula ambaye anamkubali Juma Kaseja.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic