June 1, 2018


Aliyekuwa Kocha wa KMC FC kutoka Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Fredrick Minziro, amefunguka kwa kueleza kuwa hajaona tatizo kuondolewa katika nafasi hiyo iliyochukuliwa na Mrundi, Etienne Ndayiragije.

Minziro ambaye aliipandisha daraja KMC mpaka Ligi Kuu Bara ameondolewa kwenye kikosi hicho baada ya Kocha Ndayiragije aliyewahi kuifundisha Mbao FC akichukua mikoba yake.

Kutokana na kuondoshwa kwake Minziro, ameeleza kuwa yeye amelipokea kawaida tu kutokana nafasi hiyo ina taaluma yake japo akiahidi kuelez mengi Jumanne ya wiki ijayo atakapoitisha kikao na Waandishi wa Habari.

Leo klabu hiyo imemtangaza rasmi Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu wa KMC tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikumbukwe tu kuwa Minziro aliwahi kuipandisha pia Singida United kucheza Ligi Kuu msimu wa 2016/17 lakini akaondolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm akachukua nafasi yake akitokea Yanga.

8 COMMENTS:

  1. If someone hurts you, don't feel bad, because it is a law of nature that a tree that bears sweetest fruits gets a maximum number of stones

    ReplyDelete
  2. Nadhani inategemea mkataba wake aliosaini lakini katika hali ya kawaida si busara kupuuza kazi yake. Angalau angebakia kuwa kocha msaidizi. Huyu ni mtanzania tunapaswa hata kama kocha mkuu ni kutoka nje ya nchi basi msaidizi wake awe mtanzania ili kujenga uwezo wa watanzania. Minziro kwakweli ameonewa kama hatakuwa angalau kwenye benchi la ufundi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumtetee Minziro jamani ameonewa sana. Watu toeni maoni yenu humu tupaze sauti asionewe hivi sio sahihi mbona wachezaji tunawapigania haki zao kwanini huyu mzalendo hatutaki kumzungumzia? Ila tusubiri kauli yake jumanne anasemaje.

      Delete
  3. Kwa Singida United tulinyamaza ila kwa hilo KMC haikuwa busara, pigana yote ile hadi ligi kuu, angalia Julio na maneno yake yote alishindwa kufurukuta na Dodoma FC ila Minziro pamoja na kuwa katika kundi gumu akapita leo kirahisi anaondolewa. Kwa nini hawakumshirikisha? Kwa sababu hata Meya wakati anazungumza juu ya kocha mpya hajagusia lolote kabisa hata kama mkataba umeisha angalau wangeonyesha fadhila.
    Ngoja tusubiri Jumanne atasema nini?

    Protas Iringa

    ReplyDelete
  4. tatizo ni uyanga wake ndio maana hawamtaki kuwa kocha ligi kuu wengi wanamkumbuka alivyoipa ubingwa yanga akiwa kocha wa prisons ila kwa sababu madaraja ya chini yanga haipo wanaona poa

    ReplyDelete
  5. Huyu ana upuuzi mkubwa. Akiwa team flan ikaja kucheza na yanga anauza mechi. Wamwache abaki huko huko. Ndo maana yanga safari hii ushindi ulikuwa shida sababu makocha wake wengi hawapo au team zake za kujipatia poin bure hazipo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic