June 2, 2018


Tawi moja la Yanga mkoani Mwanza limeibuka na kupiga kauli ya Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga baada ya kuibuka na kueleza kuwa anataka kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo.

Mzee huyo ameibuka hivi karibuni na kutangaza kuwa atagombea nafasi hiyo ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Yusuph Manji ambaye alijiuzulu ili kupumzika.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Kiongozi wa tawi hilo, Mhando Madega, amesema kuwa mzee huyo amekuwa mnafiki na mchochezi kwani amekuwa akiibuka pale Yanga inapokuwa haina wakati mzuri.

Aidha, Madega ameongeza kwa kueleza kuwa Akilimali hajawa na msaada wowote ndani ya Yanga zaidi ya kutupia lawama uongozi ambao umekuwa ukiipigania klabu katika nyakati zote ambazo inapitia.

Madega ameuomba uongozi wa Yanga uangalie namna ya kumsimamisha Akilimali ikiwezekana kumfuta kabisa uanachama ndani ya klabu kwani amekuwa akileta sintofahamu nyingi zisizokuwa na maana.

2 COMMENTS:

  1. Kila mwanachama wa Yanga mwenye sifa ya kugombea uongozi katika klabu anayo haki ya kutaka kugombea uongozi wa klabu yake hiyo. Tatizo lipo wapi? Hakuna haja ya kulikuza jambo dogo la wanachama wenyewe watakaoamua nani wampe kura.

    ReplyDelete
  2. hao wanachama badala ya kumtupia lawama Mzee Akilimali wangekuja na mkakati wa kuisaidia klabu kipindi hiki kigumu vinginevyo hawana faida yoyote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic