June 5, 2018



Wakati usajili wa awali kwa klabu za Ligi Kuu Bara ukiendelea hivi sasa, uongozi Yanga umefunguka na kusema hautaki kuweka wazi usajili wake.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa hawataki kuweka wazi usajili wao ili kuibiwa wachezaji.

Mpaka sasa Yanga haijatoa taarifa juu ya usajili ilioufaanya tangu kumalizika kwa msimu wa ligi wa 2017/18.

Mkwasa ameeleza kuwa Yanga hawataji majina ya wachezaji wanaotaka kuwasajili kuhofia kuchukuliwa na baadhi ya timu ambazo zinategemea ikishataja tu majina yao, inawasajili.

Kutokana na kauli hiyo, Mkwasa amewaomba wanachama na wapenzi wa Yanga kuwa na subira kwani muda utakapotimia wataweka wazi usajili wa wachezaji wapya watakaoingia nao mikataba.

6 COMMENTS:

  1. Si sasa wala si baadae. Ni jambo la ajabu daima kuficha ukweli. Si aibu hata kidoho kukubali kuwa mna shida ya pesa ambapo mna madeni ya kuwalipa wachezaji na pia munahitaji mamilioni ya usajili. Msiwe daima kisingio matatizo ya familia na wachezaji wagonjwa. Mkikiri huenda akatokea msamiria akakusaidieni ili mambo yatulie nanyi muache visingizio visivo mans

    ReplyDelete
  2. Mficha uchi hazai..
    ..tatizo ni kubwa lakini wanachama hawashirikishwi katika kutatua....sasa ngome inaendelea kumeguka kocha, viongozi, wachezaji kutosajili...
    Kumbukeni bado kuna mashindano ya CAF mechi kama nne zimebaki....lazima mfanye uchaguzi ndani ya wiki mbili, pia mteue benchi la ufundi la muda, na msajili wachezaji sio kuongea tu...lugha kama hizi hazitakiwi.
    ..tuko kwenye mpango, tunategemea, tunatafuta, tunaandika barua.....huu ni uzembe....wengine wanatoa pesa wanachukua mchezaji!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Mnahitaji kuwaacha wachezaji wabovu km mwashiuya, mahadhi, Tambwe, Kakolanya, Youthe, Ngoma yule mkongo aliyesajiliwa akala fedha halafu akakimbia na martin. Kisha kusajili Allan Wanga, Marcell Koupko, Pascal Wawa, Ley Vuy Matampi, Benedict Tinoco, Ditram Nchimbi, Boniface Maganga, Nurdin Chona, Hassan Kabunda na Peter Mapunda

    Ushauri tu

    ReplyDelete
  6. Mnahitaji kuwaacha wachezaji wabovu km mwashiuya, mahadhi, Tambwe, Kakolanya, Youthe, Ngoma yule mkongo aliyesajiliwa akala fedha halafu akakimbia na martin. Kisha kusajili Allan Wanga, Marcell Koupko, Pascal Wawa, Ley Vuy Matampi, Benedict Tinoco, Ditram Nchimbi, Boniface Maganga, Nurdin Chona, Hassan Kabunda na Peter Mapunda

    Ushauri tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic