June 1, 2018


Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kueleza kuwa hakuna mchezaji yoyote anayejuta kuwachezea mabingwa mara 27 wa ligi kuu bara.

Mkwasa amesema kuwa Yanga ni sehemu nzuri ya kuwa na wachezaji hivyo hakuna yeyote atakayeweza kujuta endapo atajiunga na kikosi cha timu yao ingawa akisema ni msimu huu tu pekee mambo yajakaa vizuri.

Katibu huyo ameeleza Yanga haijawaka na msimu mzuri kipindi hiki kutokana na kuyumba kifedha lakini anaamini kuwa klabuni kwao bado ni sehemu ambayo mchezaji anaweza akaonesha kile alichonacho.

Kauli hiyo ya Mkwasa imekuja kufuatia tetesi mbalimbali zilizoeleza kuwa itaondokewa na wachezaji wao kuelekea sehemu zingine ambazo amezikanusha kuwa hazina ukweli.

"Hakuna mchezaji anayejutaka kuichezea Yanga kwa maana ni sehemu salama ya wachezaji" amesema Mkwasa.

Mapema jana baada ya kukutana na Kelvin Yondani, Mkwasa aliyaeleza hayo na kusema kuwa hakuna ukweli wa taarifa hizo na akiomba zipuuzwe ikiwemo ya Yondani aliyehusishwa kwenda Simba pamoja na Azam FC.

4 COMMENTS:

  1. Mgomo ni dalili ya majuto kwakuwa wanaendesha maisha ya familia zao na malipo yakisita hakuna uhai. Wachezaji hawabaki katika klabu kwa mapenzi ya klabu kama ilivo zamani lakini kutafuta maisha na ikiwa hakuna maslaha huelekea kwengine

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zamani mchezaji anachagua kuchezea Yanga au Simba (Sunderland) kwa mapenzi ya Rangi ya bendera ya Klabu, iwe nyekundu au kijani. Rangi ya Bluu ni wana Cosmopolitan, timu aliyoichezea kwa mafanikio marehemu Msomali, n.k Leo hii hakuna swala la mapenzi ya rangi, kwanza ni fedha mbele. Sasa viongozi mtajidanganya kama msipotafuta fedha kuwalipawachezaji utegemee mapenzi kwa klabu bingwa mara 50, haina maana yeyote. Lakini pili, Sportspesa ndiye mfadhili wa timu za Yanga na Simba na wengine Singida n.k mbona kilio kila siku ni kwa Yanga kukosa fedha za kuhudumia wachezaji kwanini? je kuna matumizi ya ziada ambayo hayaendi kulipa wachezaji wetu?. Vizuri kuweka wazi jambo hili. Uongozi kaeni mtafakari jambo hili. Wasipolipwa wachezaji wazuri wataondoka tuu huo ndio ukweli.

      Delete
  2. Na sio hapa Tanzania na yanga yu tu bali kote duniani

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo mapenzi ya timu yawafanye watoto wa wachezaji wapate unyafuzi na kwasahaikor kwa nini msiwalipe?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic