June 1, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania Bara limetolea tena ufafanunuzi kuhusiana na Mtibwa Sugar endapo itashinda mchezo wa Kombe la Shirikisho kesho dhidi ya Singida United kama itapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Ikumbukwe Mtibwa ilifungiwa kushiriki mashindano hayo ya CAF baada ya kushindwa kusafirisha kikosi chake kuelekea nje ya nchi sababu ya ukata wa fedha ikiwa ni baada ya mwaka 2000 kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema kuwa adhabu ya waliyopewa Mtibwa Sugar tayari imeshamalizika iliyokuwa ya miaka mitatu.

Aidha, Ndimbo ameeleza kuwa kama kutakuwa na mabadiliko mengine kutoka CAF kuhusiana na Mtibwa endapo atashinda na kupata nafasi hiyo, watajua namna gani ya kufanya ili kupeleka mwakilishi.

Mtibwa anakutana na Singida United katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kesho kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuanzia majira ya saa 10 jioni.

2 COMMENTS:

  1. Msitake kuwabania Mtibwa. Adhabu imemalizika hayo mengine yatoke wapi? Na kwanini nyinyi TFF msubiri mengine yaje? Akishinda Mtibwa awakilishe nchi. Kama atazuiwa kwa hayo mengine, basi hakuna timu kuwakilisha tupoteze tu nafasi. Lazima kutenda haki. Kwanza Mtibwa kwanini aliadhibiwa kwa kushindwa nauli ya kupeleka timu Afrika Kusini wakati TFF ipo na inalo jukumu la kuhudumia timu inayowakilisha nchi? Mbona Yanga ilipowakilisha nchi mliwakatia tiketi timu ikasafiri nje baadae mnawadai taratibu kwanini hamkufanya kwa Mtibwa?

    ReplyDelete
  2. Mtibwa Sugar acha kuangalia adhabu wewe shinda mengine yatajulikana wasiwakatishe tamaa, mlipofika mnastahili taji hilo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic