June 14, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umetoa ofa kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kwa yeyote inayotaka kusajili mchezaji wake wafike mezani kufanya makubaliano.

Kupitia Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jamal Bayser, amesema kuwa wao hawana kinyonho cha kuweza kuwabania wachezaji na vilevile mpira ni biashara hivyo watasajili wengine.

Kupitia Sports Xtra ya Clouds FM, Bayser amefunguka kipindi hiki ambacho vuguvugu la usajili tayari limeshaanza akizikaribisha timu ambazo zinahitaji mchezaji kutoka klabuni kwao.

Kiongozi huyo anaamini Mtibwa ni chuo cha soka na hivyo watajitahidi kutengeneza wachezaji wengine ambao watakuwa mhimili mzuri wa timu kwa msimu ujao wa ligi.

Mtibwa imekuwa moja ya timu ambazo hutengeneza vizuri wachezaji na mwisho wa msimu unapofika imekuwa ikiwauza kuelekea mahala pengine.

Mtibwa ilifanikiwa kuwauzia Simba wachezaji wake kadhaa muhimu wakiwemo nyota Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Ibrahim Mohamed Ibrahim na Ally Shomari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV