June 2, 2018


Na George Mganga

Kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho leo Jumamosi, Nahodha wa Singida United, Nizar Khalfan, amesema mipango yao ni kupata ushindi ili kuwaikilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nahodha huyo amefunguka kwa kueleza kuwa maandalizi yao yamemalizika salama huku wakifanyia marekebisho ya mapungufu kadhaa yaliyokuwepo kwenye timu tayari kukabiliana na Mtibwa jioni ya leo.

Kwa mujibu wa Radio One, Mbali na maandalizi, Khalfan amewaambia Mtibwa wategemee ushindani wa nguvu katika mechi hiyo ambayo itakuwa sehemu ya kulipiza kisasi baada ya kufungwa katika mchezo wa ligi msimu uliomalizika kwa mabao 3-0 ikiwa kwao Namfua Stadium.

"Matarajio ya mchezo wetu ni kushinda kutokana na maandalizi ambayo tumefanya. Mtibwa wasitarajie ulaini wa mechi bali wajue wanaenda kukutana na upinzani mkubwa na si lelemama" amesema Khalfan.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka jijini Arusha, itaanza majira ya saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

1 COMMENTS:

  1. Ila Singida United mnaongea sana. Hata kwa Simba FC mlisema wakija Singida watakiona cha mtema kuni, kumbe hata Mtibwa Sugar waliwachapa kwenu na mnakumbuka. Sasa mtakuwa Arusha na hiyo timu siyo ya mchezo mchezo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic