June 24, 2018


Chama cha Wanasoka Tanzania (SPUTANZA), kimeibuka na kuelezea kiuchache kuhusiana na sakata la Stand United kuchelewesha mishahara ya wachezaji wao.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Mussa Kisoki, amesema kweli klabu hiyo imekuwa moja ya zile zinazochelewesha mishahara ya wachezaji na wamekuwa wakijitahidi kuipa elimu.

Kwa mujibu wa Radio One, Kisoki amefunguka na kueleza kuwa tatizo hilo lipo Stand kwa muda mrefu lakini wamekuwa wakijitahidi kutoa mchango wao kwa klabu hiyo.

Hatua imekuja mara baada ya beki wake, Ally Ally kueleza kuwa anaidai klabu mshahara wa ytakribani miezi mitatu ambao bado hajalipwa.

Ally alifunguka na kusema kuwa Stand imekuwa ni kawaida kutolipa mishahara wachezaji wake kitu ambacho kinatoa morali na hamasa ya wao kujituma Uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic