June 22, 2018


Baada ya awali kuelezwa kuwa ana nia ya kuitaka Yanga, beki wa zamani wa Azam FC, Pascal Wawa, ameingia kwenye rada za Simba na ikielezwa wameanza harakati za kuwapiku Yanga.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema kuwa Simba wameanza harakati za kumalizana na beki huyo aliyewahi kukipiga Azam na kisha baadaye kutimkia Al Merrick ya Sudan.

Hapo awali kulikuwa na mipango ya mabosi wa Yanga kuanzisha mipango ya kutaka kumrejesha Tanzania beki huyo lakini inaonekana wanaweza kukwama kutokana na fedha za Mo ndani ya Simba.

Ikumbukwe hivi karibuni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alinukuliwa akisema timu yao ipo kwenye mikakati mathubuti ya kuhakikisha inaleta beki wa kimataifa kuja kuongeza nguvu katika idara ya ulinzi.

Endapo Simba watafanikiwa kukamilisha dili la Wawa kutua kwenye timu yao itakuwa ni usajili wa beki wa kwanza katika msimu ukiachilia washambuliaji iliowasajili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic